Msingi katika ndoa ni kuoa wake wengi

Swali: Msingi wa ni kuoa wake wengi au mmoja tu?

Jibu: Msingi ni kuoa wake wengi:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]

Hili ndio bora. Kwa sababu kufanya hivo ndani yake kuna kuwahurumia wanawake, kufanya kizazi kikawa kikubwa, kuwalinda wanawake na machafu na kuwafanya wanaume wakawa wengi zaidi. Kila ambavo wanamme wataoa wake wengi ndivo wanaume na wanawake wanajilinda na machafu zaidi.

[1] 04:03

Check Also

Mke anadai ana maradhi baada ya mume wake kuoa mke wa pili

Swali: Kuna dada kutoka Uingereza anauliza. Mume wangu ataoa mke wa pili, kisha [huyo mwanamke] …