Msikiti kwa mwenye maradhi ya kutokwa na manii kila mara

Swali: Ndugu yangu amepatwa na hali ya maradhi kwa njia ya kwamba kwa siku moja anatokwa na manii mara kadhaa mara kwa matamanio na wakati mwingine pasi na matamanio. Wakati mwingine hali hiyo inamtokea akiwa msikitini. Ni ipi hukumu ya hali hiyo?

Jibu: Manii yakimtoka kwa matamanio basi analazimika kutoka nje ya msikiti na kuoga josho la janaba. Na manii yakimtoka pasi na matamanio basi hatolazimika kutoka nje ya msikiti na wala kuoga josho la janaba. Lakini analazimika kutawadha kutokana na hali hiyo kwa ajili ya kila swalah baada ya kujisafisha tupu na kulinda msikiti usije kuchafuka kwa yale yanayomshuka hali ya kuwa msikitini.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/351) nr. (5512)
  • Imechapishwa: 06/06/2022