Msichana kuwakatalia wazazi wake kuolewa na mwanamme asiyempenda

Swali: Wazazi wangu wamemuoza dada yangu kwa mwanamme asiyemtaka. Ni ipi hukumu ikiwa yeye mwanamke hamtaki? Akikataa anazingatiwa kuwa ametenda dhambi?

Jibu: Kinachompasa baba wakati anapotaka kumuoza mwanamme msichana wake na akamposa kwa mwanamme ambaye anafaa katika dini, tabia na amana yake na akawa na dhana kubwa ya kwamba mwanamme huyu anaendana naye, basi amdhihirishie hilo msichana wake na ambainishie sifa zake na yale ya muhimu kuyazingatia kuhusu mwanamme huyo na amfunulie hali yake kwa uwazi kabisa. Akimtaka basi ahimidiwe Allaah na asimpotaka basi haki itakuwa pamoja na msichana huyo. Hata hivyo haijuzu kwake kumlazimisha na kumuamrisha ilihali yeye msichana amechukia.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiozeshwe msichana bikira mpaka atakwe idhini.”

Haidhuru asimpomtii baba yake. Huko sio kumuasi. Hiyo ni haki yake. Yeye msichana ndiye atachomwa na moto wa mwanamme na si baba yake. Kazi ya baba ni kuozesha. Lakini ambaye ataishi na mtu huyo ni msichana. Pengine akawa na sababu za msingi zinazomfanya yeye kumkataa. Inapaswa kujua ni sababu zipi zilizomfanya msichana huyo kumkataa mwanamme huyo. Ajaribu kumuelewa kwa usahihi na kwa mazingatio na asiharakie kumpinga. Bali azingatie uchunguzi wake na atazama kama kuna uwezekano wa kuyarekebisha.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-زواج-البنت-بالإكراه
  • Imechapishwa: 06/09/2022