Msafiri kufupisha nyuma ya imamu anayeswali Taraawiyh


Swali: Kuna msafiri amejiunga pamoja na imamu mwenye kuswali Taraawiyh. Je, inakubalika Kishari´ah kwa mswaliji huyu kuswali Taraawiyh hii kwa nia ya ´Ishaa hali ya kufupisha?

Jibu: Ndio, inafaa kwake kufanya hivo. Akiwa ni msafiri na akaswali pamoja na imamu na akatoa Tasliym zitamtosha yeye Rak´ah hizo mbili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 02/03/2019