Swali: Kuna mwanamke wa Kiislamu ambaye tayari kishaolewa anaitukana dini. Je, atalikike kwa mume wake kwa sababu ya kitendo hichi? Vipi ikiwa atatubia?

Jibu: Anaritadi kutoka katika Uislamu. Mwenye kutukana dini anatoka katika Uislamu midhali akili ya mtu huyo haina kasoro. Ikiwa akili yake ina kasoro hapati dhambi. Vinginevyo anaritadi kutoka katika Uislamu. Akitubu kabla ya eda kwisha, basi bado anabaki na mke wake. Eda ikwisha na bado hajatubia, anatengana na mume wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2018