Swali: Kulitokea baina yangu mimi na mke wangu tofauti kisha siku hiyo nikampiga kutokana na ghadhabu niliokuwa nayo, akalia na kunambia “nataka unitaliki”. Nikamwambia “vaa nguo zako nikupeleke kwa familia yako”. Alipokuwa anataka kuvaa nguo zake nikawa nimemkataza kufanya hivyo na tukapatana siku hiyo hiyo kama kwamba hakukupitika kitu. Na hapo ilikuwa miezi miwili iliopita. Lakini nafsi yangu inanambia mara kwa mara mbali na muda wote huu kuhusu hukumu ya Kishari´ah kutokana na tulioambizana. Na je, kwa hayo Talaka itakuwa imepita?

Jibu: Ikiwa hali ni kama alivyosema muulizaji, hakuna Talaka, kwa kuwa nia peke yake haipitishi Talaka. Isipokuwa Talaka inapita kwa kufanya moja ya mambo mawili; ima kwa kutamka maneno au kuandika. Au nia peke yake haipitishi Talaka. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu, yanayohadithiwa na nafsi zao maadamu hawajayafanya wala kuyatamka.”

Nia peke yake wanachuoni wanaona kuwa Talaka haiwezi kupita. Kuwa na utulivu ewe ndugu na umshukuru Allaah kuwa na usalama. Na ninamuomba Allaah Atupe sote Tawfiyq.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 19/03/2018