Mke analalamika kwa mume kuwa mbali kwa muda mrefu

Swali: Kuna mwanaume kamwacha mke wake kijijini zaidi ya mwaka na bila ya udhuru unaokubalika Kishari´ah. Yeye kazi yake ni kukusanya pesa tu, kupenda dunia na kujifakharisha. Hivi sasa amemwacha kijijini kwa familia yake pasi na kujerea isipokuwa baada ya zaidi ya miezi saba. Lengo ni kukusanya pesa tu. Je, kitendo kama hichi kinafaa?

Jibu: Uhakika wa mambo ni kwamba kitendo hichi ni upumbavu kutoka kwa mtu huyu. Kwa sababu kitu muhimu zaidi ambacho mtu anaweza kukusanya katika dunia hii ni kustarehe kwa kukidhi shahawa zake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameanza kwa kuwataja wanawake kabla ya mirundi iliyorundikwa pale aliposema:

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ

“Watu wamepambiwa kupenda matamanio ambayo ni wanawake na watoto na mirundi ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa ya aina bora na mifugo na mashamba.”[1]

Sielewi ni vipi mtu huyu anaweza kusubiri muda wote huu akiwa mbali na mke wake kwa ajili ya kukusanya dunia ambayo si yenye kumnufaisha ikiwa hakuitumia kwa ajili ya kufikia starehe zake? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dunia ni starehe na starehe yake bora zaidi ni mke mwema.”

Jengine ni kwamba mwanamke huyu akiridhia kazi yake mume huyu hapati dhambi kwa sababu haki ni yake mwanamke. Isipokuwa ikiwa kule kumtelekeza kwake kunachelea juu ya mwanamke akaingia kwenye mitihani. Katika hali hiyo ni lazima kwake kumchunga mke wake. Ikiwa mke anamtaka na hayuko radhi kwa yeye kuwa mbali kwa muda wote huu mrefu basi ni lazima kwa mume kumtekelezea haki yake na asimsuse kwa safiri hii.

[1] 03:14

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (17) http://binothaimeen.net/content/6822
  • Imechapishwa: 10/09/2021