Mfungaji akifanya punyeto ni wajibu kwake kutoa kafara?


Swali: Mfungaji akifanya punyeto ni wajibu kwake kutoa kafara?

Jibu: Mfungaji akifanya punyeto na akatokwa na manii ni wajibu kwake kulipa siku hiyo ambayo amefanya punyeto. Haimlazimu kutoa kafara. Kafara sio wajibu isipokuwa kwa kufanya jimaa peke yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/233)
  • Imechapishwa: 12/06/2017