Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwaambia Maswahabah juu ya ambaye atakuwa na subira katika dini yake:

“Mbele yenu kunakuja masiku ambayo mwenye subira ni kama mfano wa aliyeshika kaa la moto na mtendaji mwenye kutenda kama nyinyi analipwa ujira wa wanaume khamsini.” Tukasema: “Katika sisi au katika wao?” Akasema: “Katika nyinyi.”[1]

Je, hii ina maana kwamba ambaye atakuwa na subira katika zama za mwisho ni mbora kuliko Muhaajiruun na Answaar?

Jibu: Wanazuoni wamejibu kwa kusema kwamba atakuwa na thawabu khamsini katika Maswahabah katika kipengele hiki peke yake kwa kule kuwa kwake na subira licha ya kuonekana mgeni. Maswababah walikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waliokuwa wakimnusuru walikuwa wengi katika wakati wao. Lakini mtu huyu katika zama za mwisho anaonekana ni mgeni kati ya watu. Licha ya hivo akasubiri na kuwa imara. Kutokana na sifa hii akapata thawabu za Maswahabah khamsini. Kuhusu Maswahabah wao wako na sifa nyingi. Wao pasi na shaka ni wabora kuliko wengine kutokana na sifa nyingi. Ubora maalum haupelekei kushinda fadhilah zilizoenea, kama inavosema kanuni.

[1] at-Tirmidhiy (3058).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 35
  • Imechapishwa: 14/05/2021