Swali: Imepokelewa katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoonyeshwa nyumati mbalimbali akaona Ummah wake kuwa ni kikundi kikubwa[1]. Vipi tutaoanisha hilo na hali yetu hivi sasa kwa njia ya kwamba ni wachache wanaofata mfumo ambao ni sahihi?

Jibu: Mkusanyiko wa watu wote kuanzia hapo Allaah alipomtuma Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka kusimame Qiyaamah ni wengi. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mwenye wafuasi wengi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna katika Manabii Nabii yoyote isipokuwa alipewa kiasi cha vile walivyomwamini watu… “

Bi maana katika miujiza.

“… hakika si venginevyo kile alichopewa ni Wahy ambao Allaah amemteremshia…”

Bi maana Qur-aan.

“Nataraji mimi ndiye ambaye nitakuwa na wafuasi wengi katika wao.”[2]

Mkusanyiko wa watu wote kuanzia pale Allaah alipomtuma Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka kusimame Qiyaamah watakuwa wengi. Ijapo baadhi ya zama wanaweza kuwa wachache na baadhi ya zama zengine wakawa wengi.

[1] al-Bukhaariy (4981).

[2] al-Bukhaariy (4981).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 14/05/2021