Mavazi yenye kubana kati ya wanawake wenziwe

Swali: Wanawake wengi wanavaa mavazi ya sketi na blauza na yanakuwa yenye kubana kidogo lakini si yenye kuonyesha kwa ndani na si mafupi. Ni ipi hukumu ya mavazi haya?

Jibu: Mwanamke wa kiislamu anatakiwa kumcha Allaah juu ya mavazi yake na mavazi yake yawe yenye kusitiri na yasiwe yenye kuonyesha ndani bi maana yawe mazito. Mwanamke amche Allaah kwa yale anayovaa. Mwanamke anatakiwa kujihadharia. Ni mamoja anatoka kuwaendea wanamme hata katika jamii za wanawake wenzie. Pengine akafikwa na kijicho cha wanawake wenye husuda na kijicho cha wanawake wenye chuki. Kujisitiri na kujiheshimu ni miongoni mwa sababu za utukufu wake na watu kumuheshimu na watenda maasi na waasherati kutothubutu dhidi yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-لبس-الملابس-الضيقة-للنساء
  • Imechapishwa: 11/06/2022