Masikini wanataka Zakaat-ul-Fitwr wapewe pesa badala ya chakula

Swali: Katika mji wetu Zakaat-ul-Fitwr kunatolewa pesa kwa hoja ya kwamba masikini hawataki nafaka au kitu kingine. Tufanye nini?

Jibu: Wenye kuamua sio masikini. Hii ni ´ibaadah. Inatakiwa kutekelezwa kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule asiyetaka chakula sio muhitaji. Badala yake wape wahitaji ambao wanataka chakula.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/12939
  • Imechapishwa: 21/06/2017