Mashambulizi Ya Kigaidi Paris Hayakubaliwi Na Uislamu


Sekretaria mkuu wa baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa Saudi Arabia amekea mashambulizi ya kigaidi ambayo yametokea mji mkuu wa Ufaransa Paris ambayo yamepelekea watu wengi kupoteza maisha yao na kujeruhiwa.

Sekretaria mkuu wa baraza ameashiria kuwa mashambulizi haya ya kigaidi hayakubaliwi na Uislamu na yanaenda kinyume na thamani yake ambayo ni rehema kwa walimwengu. Imebainisha kuwa sawa mashambulizi haya ya kigaidi na mengineyo ni muendelezo wa ugaidi ambao serikali ya kihalifu ya Syria na wasaidizi wake wanawasababishia raia wa Syria mabomu mazito. Kutoka kwenye serikali hii kumetoka ISIS, kikundi cha kigaidi ambacho kinafanya hadaa kwa serikali ya Bashshaar. Ulimwengu kuwafumbia macho ndio yamepelekea kutokea matendo haya ya jinai yanayofanyika.

Sekretaria mkuu amebainisha pia kuwa ugaidi unatakiwa kutokomezwa kwa kupambana na makundi yote ya kigaidi pasi na kujali ni kundi gani la kigaidi linachangia kutoa kitu katika manufaa.

  • Mhusika: Kibaar-ul-´Ulamaa'
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alarabiya.net/ar/saudi-today/2015/11/14/%D9%87%D9%8A%D8%A6%D8%A9-%D9%83%D8%A8%D8%A7%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B9%D9%84%D9%85%D8%A7%D8%A1-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D8%B9%D9%88%D8%AF%D9%8A%D8%A9-%D8%AA%D8%AF%D9%8A%D9%86-%D9%87%D8%AC%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D8%A8%D8%A7%D8%B1%D9%8A%D8%B3.html
  • Imechapishwa: 07/02/2017