356 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Jibriyl (´alayhis-Salaam) alinijia akasema: ”Nilikuwa nimekujia jana usiku. Hakuna kilichonizuia kuingia ndani ya nyumba uliyokuwemo isipokuwa ni kwamba kulikuwa na kinyago cha sanamu cha mwanamme. Katika nyumba kulikuweko kinyago cha sanamu katika pazia. Amrisha kichwa cha kinyago hicho kikatwe kiwe na umbile kama la mti. Amrisha pazia ikatwe na kufanywe mito miwili inayokanyagwa chini[1]. Amrisha mbwa atolewe nje.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanya hivo. Mbwa huyo alikuwa ni kilebu cha al-Hasan na al-Husayn kilichokuwa chini ya kitanda chao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Hakuacha kuendelea kuniusia juu ya jirani mpaka nikafikiri kuwa atamfanya kunirithi.”

Ameipokea Ahmad (2/305) na tamko ni lake, Abu Daawuud (4158), at-Tirmidhiy (2/132) na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” (1487) kupitia kwa Yuunus bin Abiy Ishaaq, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mutme wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim na pia imesahihishwa na at-Tirmidhiy na wengineo…

Mafunzo katika Hadiyth:

1- Picha ni haramu na ni sababu inayowazuia Malaika kuingia nyumbani. Hadiyth kuhusu uharamu wake zimetangaa kiasi cha kwamba hakuna haja ya kuzitaja.

2- Uharamu unakusanya picha ambazo si za aina ya kiwiliwili wala za kivuli kutokana na ueneaji wa maneno ya Jibriyl (´alayhis-Salaam):

”Sisi hatuingii ndani ya nyumba zilizo na kinyago.”

Kinyago ndio picha zenyewe, kinachotilia nguvu hilo ni kwamba kinyago kilichoko katika pazia hakina kivuli. Hakuna tofauti kati ya picha zilizoko kwenye nguo kama mapambo, uchoraji kwenye karatasi au kwa mashine ya kupiga picha. Kwani zote hizo ni picha na utengenezaji picha. Kutofautisha kati ya picha zinazochorwa kwa mkono na picha za mashine ya kupiga picha ambazo za sampuli ya kwanza zinaharamishwa tofauti na sampuli ya pili ni mfano wa muonekano wa kisasa na usiokuwa na uhai wenye kusemwa vibaya.

[1] Katika upokezi mwingine imekuja:

”Katika nyumba kuna pazia ilio na kinyago. Ondosha kichwa chake na uifanye busati au mto unaokanyagwa. Hakika sisi hatuingii katika nyumba zilizo na vinyago.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadîth as-Swahiyhah (1/2/691-693)
  • Imechapishwa: 27/08/2020