Majini wako matabaka mbalimbali kama watu

Swali: Ni ipi lugha za majini?

Jibu: Dhahiri ni kwamba wao ni kama watu. Wana lugha mbalimbali. Miongoni mwao wako wangereza, wafaransa, wamarekani, waajemi na waaramu. Matabaka mbalimbali. Allaah amesema juu yao:

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَائِقَ قِدَدًا

”Na kwamba wako katika sisi wema na wako katika sisi kinyume na hivo; tumekuwa makundi ya njia mbalimbali.”[1]

Wako makundi mbalimbali.

وَأَنَّا مِنَّا الْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا الْقَاسِطُونَ

“Na kwamba wako katika sisi waislamu na wako katika sisi wakengeukaji haki.”[2]

Miongoni mwao makundi mbalimbali. Miongoni mwao wako wema na wengine wabaya. Miongoni mwao wako wanaopinga majina na sifa za Allaah, Sunniy, Raafidhwiy, wakristo, mayahudi na wengineo. Wako makundi na mapote mbalimbali.

وَأَنَّا مِنَّا الصَّالِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ

”Na kwamba wako katika sisi wema na katika sisi kinyume na hivo.”[3]

Hii imekusanya makundi mengine.

[1] 72:11

[2] 72:14

[3] 72:11

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/7591/%D8%A8%D9%8A%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%86-%D9%84%D9%84%D8%AC%D9%86-%D8%B9%D8%AF%D8%A9-%D9%84%D8%BA%D8%A7%D8%AA-%D9%83%D9%85%D8%A7-%D9%87%D9%8A-%D9%84%D8%A8%D9%86%D9%8A-%D8%A7%D8%AF%D9%85
  • Imechapishwa: 16/05/2020