Furaha ya mfungaji atapokutana na Mola Wake

Kuhusu furaha ya mfungaji wakati atapokutana na Mola Wake ni kutokana na zile thawabu nyingi za funga atazozikuta mbele ya Allaah wakati ambapo ndio atakuwa na haja zaidi kuliko wakati mwingine. Amesema (Ta´ala):

وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّـهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا

“Na chochote kile mnachotanguliza katika kheri kwa ajili ya nafsi zenu, mtakikuta kwa Allaah ni bora na ujira mkubwa zaidi.”[1]

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا

“Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika kheri yamehudhurishwa.”[2]

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ

“Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe ataiona, na yule atakayetenda shari uzito wa chembe ataiona.”[3]

[1] 73:20

[2] 03:30

[3] 99:07-08

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Latwaa’if-ul-Ma´aarif, uk. 157
  • Imechapishwa: 16/05/2020