Majini hawakutumiwa Mtume mwingine zaidi ya Muhammad?

Ibn-ul-Qaasim amesema hakuna Mtume aliyetumwa kwa majini na watu isipokuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Lakini hata hivyo hili liko mbali. Kwa kuwa udhahiri wa maneno Yake (Ta´ala):

يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَى

“Enyi watu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Muusa.” (46:30)

ni kwamba Muusa alitumwa kwao. Vilevile maneno Yake (Ta´ala):

يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ

“[Siku ya Qiyaamah wataambiwa]: “Enyi wenzi wa majini na wanadamu! Je hawajakufikieni Mtume miongoni mwenu.” (06:130)

ni dalili yenye kuonesha kuwa walitumiwa Mitume.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/149)
  • Imechapishwa: 31/05/2020