Madhehebu haya saba yote ni batili. Haya ndio madhehebu yenye kuzunguka ulimwenguni. Lakini hata hivyo madhehebu haya hayakuenea sana. Tumeyaraddi. Madhehebu yalioenea kwa wingi ni Ashaa´irah na Kullaabiyyah. Madhehebu haya mawili yanakaribia kuwa mamoja. Wanachuoni wengi wa Fiqh na wengine, katika Hanaabilah na wengine, wameathirika na madhehebu ya Ashaa´irah. Hanafiyyah wengi vilevile madhehebu yao ni Ashaa´irah. Mwandishi wa “al-Ruudhw al-Murbiy´” mwanzoni alipoanza kusherehesha:

بسم الله الرحمن الرحيم

“Bismillaahi Rahmaan – Kwa jina la Allaah, Mwingi wa huruma”

Amefasiri “Rahmah” kuwa ni neema. Huu ni mfumo wa Ashaa´irah. Neema sio rehema.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/170)
  • Imechapishwa: 31/05/2020