Maiti hulakiniwa kabla au baada ya kufa?

Swali: Ni lini hulanikiwa maiti?

Jibu: Anayetaka kufa analakiniwa “Laa ilaaha illa Allaah”. Hivyo ndivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomfanyia ami yake Abu Twaalib pindi mauti yalipomjia. Alimwambia:

“Ami yangu! Sema “Laa ilaaha illa Allaah” ni maneno nitayokutetea kwayo mbele ya Allaah.”” al-Bukhaariy (1360) na Muslim (39).

Lakini hata hivyo ami yake Abu Twaalib hakuyatamka na hatimaye akafa juu ya shirki.

Kuhusu kumlakinia baada ya kufa ni Bid´ah. Hakukuthibiti Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo. Kinachotakiwa kufanywa ni yale yaliyopokea Abu Daawuud ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akimaliza kumzika maiti husimama mbele yake na kusema:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti. Hakika hivi sasa ataulizwa.” Abuu Daawuud (3221).

Ama kusoma na kulakini kwenye kaburi ni Bid´ah isiyokuwa na asli10.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/74-75)
  • Imechapishwa: 17/06/2017