Madhiy yanapoingia kwenye nguo au mwili

Swali: Mimi ni mtu ambaye mara kwa mara natokwa na madhiy. Je, ni lazima kwangu pindi ninapotokwa na madhiy kuosha nguo zangu kwa sababu inakuwa vigumu kwangu kujiepusha nayo?

Jibu: Ndio, ni lazima kurashia [maji juu yake]. Madhiy ni najisi nyepesi. Inatosha kurashia. Lakini ni lazima kuosha dhakari na uke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Osha dhakari na uke wako.”

Hekima – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kuepusha [madhara] katika mijira ya kutolea mkojo. Kwa hivyo nguo ikipatwa na kitu basi inatakiwa kurashiwa maji.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 04/07/2021