Maandamano na migomo ni kueneza ufisadi katika ardhi


Swali: Je, maandamano na migomo ni katika kufanya Da´wah, kutengeneza na kuonesha ghera?

Jibu: Hapana, huku ni kueneza ufisadi katika ardhi na wala hakuna yanayotengeneza wala wema wowote. Ikiwa tutasema kwamba maandamano haya hayana uharibifu wowote ule, basi itapelekea watu kutomdhukuru Allaah. Kuna khatari kukawa uharibifu, hata kama hawakukusudia hivyo.

Mkusanyiko wa kwanza wa maandamano katika Uislamu, yalisababisha shari na janga katika Ummah wa Kiislamu. Yalisababisha kuuawa kwa kiongozi muongofu ´Uthmaan ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alishuhudia kwamba ni katika watu wa Peponi.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ibnbaz.se/Artiklarna/001-100/037.html
  • Imechapishwa: 05/09/2020