Maafikiano juu ya uharamu wa muziki na nyimbo

Swali: Je, ni sahihi yale wanayosema baadhi yao kwamba muziki ni miongoni mwa mambo yaliyonyamaziwa na Shari´ah na kwamba hakukuthibiti Hadiyth yoyote Swahiyh wala Aayah ilio wazi inayoharamisha?

Jibu: Kuna maafikiano juu ya uharamu wa muziki. Hayo yamesemwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Kuna maafikiano juu ya uharamu wake. Asiwepo yeyote atakayesema kuwa umeruhusiwa. Kwa sababu ni katika ala za muziki. Kuna maafikiano juu ya uharamu wa ala za muziki, kama anavosema Shaykh-ul-Islaam.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 15/09/2018