Limiminie maji shamba lako utakavyo

Kuna mtu mmoja alisema:

“Laiti ningejua anachosema an-Nasaa´iy kuhusu kumwingilia mwanamke kwa nyuma.” Akaulizwa juu ya hilo ambapo akajibu: “Mvinyo ni haramu na kuhusu kujamii kwa nyuma hakujasihi kupokelewa chochote juu ya hilo. Lakini Muhamad bin Ka´b al-Qaradhwiy amesimulia kupitia kwa Ibn ´Abbaas ambaye amesema:

“Miminia maji shamba lako utakavyo.”

Haitakiwi kuyavuka maneno yake.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameharamisha kuwaingilia wanawake kwa nyuma kwa njia nyingi kiasi cha kwamba haiyumkiniki kuyafumbia macho. Uharamu juu ya hilo uko wazi. Nimetunga kitabu kikubwa juu ya maudhui hayo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/127)
  • Imechapishwa: 11/10/2020