La kufanya usipoweza kuwaraddi wahalifu


Swali: Ni ipi njia sahihi ya kutahadharisha juu ya walinganizi waovu?

Jibu: Ikiwa una elimu na uwezo wa kuraddi utata wao, unatakiwa kubainisha hili bila ya kusababisha fitina na athari mbaya. Fanya hivo kwa hekima, maneno mazuri na kujadiliana nao kwa nia nzuri. Na ikiwa huna uwezo huo, wafikishie wanachuoni na watawala wanaoweza kusimamia jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Tahdhiyr min Du´aat-is-Suu'
  • Imechapishwa: 05/09/2020