Kwanini wakeze Mtume wakafanywa ni mama wa waumini?


Swali: Ni kwa nini wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameitwa kuwa ni ´mama wa waumini`?

Jibu: Wameitwa kuwa ni mama wa waumini kwa sababu ya heshima na kuadhimishwa. Umama huu haupelekei katika uharamu au uhalali wowote mbali na heshima. Ni lazima kwa waislamu kuwaheshimu. Kwa sababu wao ni mama zao.

Kuhusu kuharamika kuwaoa baada ya kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hilo ni kwa sababu ya kutukuza heshima ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakeze sio halali kwa yeyote baada yake maishani. Kwa ajili hii Shari´ah imefanya miezi minne na siku kumi kwa yule aliyefiwa na mume wake kwa ajili ya kuheshimu haki mume wake aliyekufa. Hayo ni miongoni mwa haki za yule maiti. Dalili ya hilo ni kwamba mwanamke atakaa eda miezi minne na siku kumi. Muda huu ni kuhusu yule mwanamke mwenye kupata hedhi na yule ambaye hedhi yake imeshakatika. Haikupokelewa juu ya jambo hili kwamba mjamzito eda yake inakwisha anapokufa mume wake isipokuwa ni pale anapojifungua hata kama ni chini ya miezi minne. Kwa sababu tunasema kuwa pale tu ambapo eda itakwisha amekwitengana na mume na hivyo mume hana mafungamano yoyote naye. Kwa ajili hiyo eda inakwisha kwa kujifungua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6795
  • Imechapishwa: 16/02/2021