Kwa nini asikufurishwe anayerudisha nyuma maneno ya Mtume kwa kutumia akili?

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kurudisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema kuwa akili haiyakubali?

Jibu: Tunamuomba Allaah aya. Hii ni kufuru. Mwenye kusema katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuna kitu ambacho akili haikikubali, huyu ni mkanamungu. Isipokuwa ikiwa kama ni mjinga na anawaiga watu wenye kusema hivi na anawafuata kipofu, huyu anatakiwa kubainishiwa. Ama akiwa ni msomi na amekusudia kufanya hivi, kwa njia ya kwamba anaitanguliza akili – kwa madai yake – juu ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hii ni kufuru.

Akili timamu haipingani na andilo sahihi hata siku moja. Hii ni kanuni. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) anasema:

“Akili timamu haipingani na andilo sahihi. Vikitofautiana, basi ima akili sio timamu au andiko ndio sio sahihi.”

Ama kusema kwamba kuna akili timamu na andiko sahihi vinapingana, hapana. Hii ni kanuni iliosalimika kwa wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14759
  • Imechapishwa: 28/06/2020