Kuwabusu dada wa kuchangia ziwa, mama, shangazi na Mahram wengine

Swali: Ni ipi hukumu ya kupeana mikono na kuwabusu dada wa kuchangia ziwa moja?

Jibu: Mtazamo wangu juu ya dada wa kuchangia ziwa moja ni uharamu wa kuoana nao na faragha za kiharamu kama ilivyo dada wa damu. Kujengea juu ya hili inafaa kwa mwanaume kupeana mikono na dada yake wa kuchangia ziwa moja kama inavyofaa vilevile kupeana mikono na dada yake wa damu.

Kuhusu kuwabusu haitakikani kuwabusu kina dada. Ni mamoja wa damu moja wala wa kuchangia ziwa moja. Akitaka kuwatukuza au wakati ametoka safarini na mfano wake awabusu kwenye paji la uso na juu ya kichwa. Ama kumbusu mdomoni baadhi ya wanachuoni wamelikemea kwa ukali sana na wakasema kwamba ni jambo lisilotakiwa isipokuwa kwa mke tu. Hapana shaka kwamba hisia za mtu kwa wale Mahram zake juu ya dada zake wa damu moja ni tulivu zaidi kuliko dada zake wa kuchangia ziwa. Jambo hili khaswa pale ambapo dada zake wa kuchanganyia ziwa moja wanakuja kwao kwa uchache. Katika hali hii wanaweza kuwa kama wanawake wa kigeni kwa mtu huyu. Kwa ajili hii ndio maana mtu anatakiwa kujichunga zaidi katika kupeana nao mikono na kuwabusu vichwa na paji zao za uso.

Muulizaji: Umesema kuwa kubusu mdomoni ni jambo lisilotakikana isipokuwa kwa mke tu. Vipi kuhusu mama na shangazi?

Jibu: Mama, shangazi na Mahram wengine wote mtu awabusu kichwani na kwenye paji la uso. Kufanya hivi ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (09) http://binothaimeen.net/content/6723
  • Imechapishwa: 18/11/2020