Kutoa swadaqah kwa kuswali na kikosi cha watu mara ya pili

Swali: Mtu akiswali swalah ya Fajr katika jamaa´ah inajuzu kwake kuiswali mara ya pili katika jamaa´ah ya pili na akawa imamu?

Jibu: Hapana. Lakini lau atakuja mtu baada ya watu wamekwishaswali na akahitajia wa kuswali pamoja naye, hakuna neno. Ama wao wakishakuwa kundi tayari, usiingie pamoja nao kwa kuwa hawana haja na wewe. Vilevile usiswali swalah ya sunnah baada ya Fajr.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14221
  • Imechapishwa: 17/11/2014