Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa X.

Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh

Wa ba´d:

Narejelea swali lako ulilowauliza Kibaar-ul-´Ulamaa´ wa nambari 5917 tarehe 25/08/1409 ambapo umeuliza maswali kadhaa.

Napenda kukujuza kwamba inasihi kutoa adhaana na kukimu pasi na twahara. Hata hivyo bora ni mwadhini na mwenye kukimu awe na twahara. Vivyo hivyo swalah ni sahihi ijapo mwadhini na mwenye kukimu hayuko katika hali ya twahara. Mwadhini na mwenye kukimu wakiswali katika hali isiyokuwa na twahara basi atalazimika kuirudia swalah yake kama mwengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/338)
  • Imechapishwa: 18/09/2021