Swali 09: Kuna wanaosema:

“Kutikisika mara tatu kunaharibu swalah.”

Je, ni jambo lina dalili? Je, mtu anaweza kutumia dalili kwa Hadiyth ya Umaamah ambapo ndani yake inasema kwamba siku moja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu na huku amembeba Umaamah binti wa binti yake Zaynab. Kwani alipokuwa akisujudu humweka chini na akisimama humbeba[1]?

Jibu: Ni jambo halina dalili. Muislamu anatakiwa kujipa jibu mwenyewe. Akitikisika mara nyingi na yeye mwenyewe akahisi hilo  ndani ya nafsi yake basi swalah yake inaharibika.

Kuhusu Hadiyth ya Umaamah huku ni kutikisika kwa nyakati mbalimbali na si kwa kufululiza. Kumbeba kwake na kumtia chini ni jambo ambalo hakulifanya kwa kufuatanisha.

[1] al-Bukhaariy (516) na Muslim (543)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 20/09/2018