Kutabarruk kwa majasho ya mwanachuoni

Swali: Je, inajuzu kutabarruk kwa majasho ya mwanachuoni aliye hai au kitu chake kingine?

Jibu: Hakutabarrukiwi kwa majasho ya yeyote isipokuwa majasho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Majasho, mate, nywele na maji ya wudhuu´ haya ni mambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusiana na wengine haijuzu.

Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakutabarruk kwa majasho ya Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum). Hawakufanya hivo pamoja na kuwa hawa ndio watu wabora kabisa katika Ummah. Hawakutabarruk kwa majasho yao kwa kuwa haya ni mambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (08) http://alfawzan.af.org.sa/node/2123
  • Imechapishwa: 02/07/2020