Hapa ndipo mtu unaweza kuswali Witr mchana

Swali: Hujitahidi kuswali Witr katika wakati wake kabla ya kuingia kwa alfajiri. Lakini wakati mwingine nashindwa kuiswali kabla ya alfajiri kuingia. Je, inajuzu kwangu kuswali Witr baada ya alfajiri kuingia?

Jibu: Alfajiri ikishaingia na wewe bado hujaswali Witr huwezi kuswali Witr tena. Unachotakiwa kufanya ni wewe kuswali Rak´ah nne ikiwa umezowea kuswali Witr nne, Rak´ah sita ikiwa umezowea kuswali Witr tano. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapopitwa na swalah ya usiku basi anaswali mchana Rak´ah kumi na mbili[1].

[1] Muslim (746).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/114)
  • Imechapishwa: 17/06/2017