Kuswali nyuma ya imamu anayesoma Qur-aan kwa maqaamaat


   Download

Swali: Inajuzu kuswali nyuma ya anayesoma Qur-aan kwa utungo na anaipamba sauti yake kwa maqaamaat?

Jibu: Haijuzu. Maqaamaat ni katika istilahi za waimbaji. Haijuzu kuifanya Qur-aan nyimbo na kanuni za nyimbo. Hili ni haramu na haijuzu. Ikiwa anafanya hivi na nyinyi mna uhakika basi msiswali nyuma yake. Lakini iwe baada ya kumkataza. Mkimkataza na asiache jambo hili, msiswali nyuma yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014