Kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora zaidi

Swali: Mimi ni mwanafunzi mwanamke ninayesoma shuleni. Je, inajuzu kuchelewesha swalah ya Dhuhr mpaka ninaporudi nyumbani pamoja na kuzingatia ya kwamba wakati mwingine nafika 01.30?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo ikiwa umeshughulishwa na masomo na haikukuwia wepesi kwako kuswali swalah mwanzoni mwa wakati. Hakuna neno. Wakati wa Dhuhr ni mpana. Ikiwa unaswali nyumbani kabla ya wakati kutoka nje ni sawa. Ikiwa kuna wepesi wa kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziy bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=1238&PageNo=1&BookID=5
  • Imechapishwa: 15/03/2018