Kusoma Qur-aan nyumbani baada ya Fajr mpaka jua lichomoze

Swali: Nikikaa nyumbani baada ya swalah ya Fajr nasoma Qur-aan mpaka jua lichomoze kisha mtu akaswali Rak´ah mbili za Shuruuk anapata ujira uleule kama ambaye amekaa msikitini?

Jibu: Kitendo hichi kina kheri nyingi na ujira mkubwa. Lakini udhahiri wa Hadiyth zilizopokelewa katika hayo zinazonyesha kwamba ambaye ataswali mahali pake pa kuswalia hapati ujira uleule kama ambaye ameahidiwa anayeswali msikitini. Lakini ikiwa ataswali nyumbani kwake kwa sababu ya ugonjwa au khofu kisha akaketi mahali pake pa kuswalia hali ya kumtaja Allaah au akisoma Qur-aan mpaka jua likachomoza kisha akaswali Rak´ah mbili, hapo ndipo anapa ujira uliopokelewa katika Hadiyth. Kwa sababu huyu amepewa udhuru kwa kuswali kwake nyumbani.

Vivyo hivyo mwanamke akiketi mahali pake pa kuswalia baada ya swalah ya Fajr hali ya kumtaja Allaah au akasoma Qur-aan mpaka jua likachomoza kisha akaswali Rak´ah mbili, basi anapata ujira huo ambao umepokelewa katika Hadiyth. Ujira wenyewe ni kwamba Allaah anamwandikia mwenye kufanya hivo ujira wa hajj na ´umrah vikamilifu. Hadiyth juu yake ni nyingi ambapo zinapeana nguvu. Ni miongoni mwa aina ya Hadiyth ambazo ni nzuri kutokana na nyenginezo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/403)
  • Imechapishwa: 12/11/2021