Swali: Kuna watu Suufiyyah katika mji wetu wanasoma historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanamswalia na wanafanya Tawassul kwa kisomo hichi. Je, kufanya haya kunazingatiwa ni katika matendo mema?

Jibu: Hii ni Bid´ah. Kusoma historia ya Mtume sahihi ni kitendo chema kwa ajili ya kumuiga. Lakini hata hivyo kisikhusishwe katika siku ya kuzaliwa kwake au katika wakati maalum wala mtu asikusudie katika hili kufanya Tawassul kwa kisomo hichi. Kwa sababu hii ni Bid´ah. Vipi mtafanya Tawassul kwa Allaah kwa Bid´ah? Haijuzu.

Kuhusiana na kusoma historia yake katika wakati wowote muafaka kwa ajili ya kufaidika na kumuiga ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (38) http://alfawzan.af.org.sa/node/2146
  • Imechapishwa: 13/07/2020