Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy 02

83 – Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Ismaa´iyl na wengine wametukhabarisha: Ibraahiym bin Mujashshir ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia, kutoka kwa al-Hajjaaj, kutoka kwa Makh-uul, kutoka kwa Kathiyr bin Murrah aliyesema:

“Usiku huo Allaah husamehe dhambi isipokuwa za mshirikina au mwenye chuki.”[1]

Ibn-ul-Mubaarak amesimulia kutoka kwa al-Hajjaaj ambaye amemsikia al-Awzaa´iy akifasiri chuki  kwa kusema:

“Ni kila mtu wa Bid´ah ambaye kafarikiana na Ummah wake kwa Bid´ah hiyo.”

[1] Ni kama cheni iliotangulia, al-Hajjaaj kutoka kwa Mak-huul. Hapa ameweka wazi kwamba kamsikia tu al-Awzaa´iy alifasiri chuki.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 166
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy