Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy

Kuhusu upokezi wa al-Hajjaaj bin Artwa’ah kutoka kwa Mak-huul, amesema:

82 – Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Nilimsikia Muhammad bin ´Abdil-Malik al-Waasitwiy akisema na al-Qaasim bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Abu ´Ubayd ametuhadithia: al-Hasan bin Yahyaa al-Jurjaaniy ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-Hajjaaj ametuhadithia, kutoka kwa Makh-uul, kutoka kwa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy ambaye kaeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini usiku wa nusu Sha´baan na akawasemehe wa kuwasemehe isipokuwa mshirikina au mwenye chuki.”[1]

[1] al-Hajjaaj bin Artwa’ah alikuwa mdanganyifu. Anasimulia kutoka kwa Mak-huul pasi na kuweka wazi namna gani.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 158
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy