´Abdur-Rahmaan al-Muhaaribiy amesimulia tofauti.

81 – Muhammad bin al-Qaasim bin Zakariyyaa’ al-Muhaaribiy ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad al-Ahmasiy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan al-Muhaaribiy ametuhadithia…

Pia Sahl Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Hasan bin ´Aliy bin Shabiyb ametuhadithia: Nimemsikia ´Amr bin ´Uthmaan bin Abaan akisema: ´Abdur-Rahmaan bin Muhammad al-Muhaaribiy, kutoka kwa al-Ahwas bin Hakiym, kutoka kwa al-Muhaasir bin Habiyb, kutoka kwa Mak-huul, kutoka kwa Abu Tha´labah al-Khushaniy ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huwatazama waja Wake katika kila usiku wa nusu Sha´baan ambapo akawasamehe waumini, akawapa muhula makafiri na akawaacha wenye chuki na chuki zao mpaka waachane nazo.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 04/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy