80- Ahmad bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Hasan bin ´Aliy bin Shabiyb ametuhadithia: Nilimsikia ´Amr bin ´Uthmaan akisema: Muhammad bin Harb ametuhadithia: al-Ahwas bin Hakiym ametuhadithia, kutoka kwa al-Muhaajir[1] bin Habiyb, kutoka kwa Abu Tha´labah al-Khushaniy aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huwatazama waja Wake katika kila usiku wa nusu Sha´baan ambapo akawasamehe waumini, akawapa muhula makafiri na akawaacha wenye chuki na chuki zao mpaka waachane nazo.”

[1] al-Albaaniy amesema:

”Imetajwa Muhaajir lakini inatakiwa iwe Muhaasir. Ni kosa la uandishi na huja mara nyingi jina hili.” (as-Sunnah (511) ya Ibn Abiy ´Aaswim)

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 160
  • Imechapishwa: 04/05/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy