Kusema kwamba theluthi ya mwisho ya usiku ni wakati wa kushuka rehema za Allaah

Swali: Ni ipi hukumu kuhusu theluthi ya mwisho ya usiku kwamba ndio wakati zinapoteremka rehema za Allaah? Je, huku kunazingatiwa ni kupindisha sifa ya Allaah ya kushuka?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni mtu kusema kwamba ni wakati wa kushuka kwa Allaah. Theluthi ya mwisho ya usiku ni wakati wa kushuka kwa Allaah. Hivi ndio sawa. Rehema zinashuka katika kila wakati. Lakini wakati huu ni wakati ambao du´aa inaitikiwa. Ni wakati mtukufu na mbora.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/28/%D8%AA%D8%B3%D9%85%D9%8A%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AB%D9%84%D8%AB-%D8%A7%D9%84%D8%A3%D8%AE%D9%8A%D8%B1-%D8%A8%D9%88%D9%82%D8%AA-%D8%AA%D9%86%D8%B2%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AD%D9%85%D8%A7%D8%AA
  • Imechapishwa: 25/01/2020