Kusema “Astaghfir Allaah” ndani ya swalah katika kukosea kisomo

Swali: Je, inajuzu kwangu kusema:

أستغفر الله

“Nisamehe Allaah.”

nikikosea katika kisomo wakati wa swalah?

Jibu: Hapana, usiseme hivo. Usizidishe katika swalah kitu ambacho hakikuthibiti. Sahihisha kisomo chako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014