Kurudilia hifdhi ya Qur-aan makaburini

Swali:  Je, kuna ubaya na imeruhusiwa kusoma Qur-aan makaburini, sio kwa ajili ya kuwasomea maiti, bali ni pale kunapokuwa na wakati wa kusubiri jeneza ndipo nikarudilia yale niliyoyahifadhi?

Jibu: Haitakikani kufanya hivi. Kwa kuwa huku ni kufungua mlango pale ambapo mtu atakusikia aje kusema kuwa kusoma Qur-aan makaburini ni jambo linalojuzu[1]. Usisome makaburini.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/tofauti-iliyopo-juu-ya-kusoma-qur-aan-makaburini/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2120
  • Imechapishwa: 24/07/2020