Kuporomosha mimba ya mwezi mmoja baada ya kuamua kuachana

Swali: Nina mke ambaye ana mimba ya mwezi mmoja ambaye hanipendezi. Nimenuia kumtaliki. Je, inafaa kwetu kuporomosha mimba hii kwa sababu hatutaki kuendelea kuishi pamoja?

Jibu: Haijuzu kwenu kufanya hivo. Huenda mtoto huyu Allaah akawanufaisha kupitia yeye. Msiiporomoshe. Bali ni neema kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (96) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahthat-12021440h.mp3
  • Imechapishwa: 26/05/2019