Swali: Katika nchi yetu ni jambo lililoenea kwa mwanaume kupeana mikono na wanawake ambao wameharamika kwake. Je, nina dhambi kwa kuwapa mikono wanawake watuwazima ambao ni ndugu zangu nikichelea ususuwavu.

Jibu: Haijuzu kwa mtu kupeana mkono na mwanamke ambaye sio Mahram wake. Haijalishi kitu hata kama ni mtumzima. Kwa sababu mambo ni kama ilivyosemwa, kila chenye kuanguka kina mwenye kukiokota. Huenda kweli mwanamke akawa mtumzima lakini hata mwili wake ukawa bado ni kama wa msichana. Hivyo kukapatikana fitina. Kwa kifupi jibu ni kuwa: haijuzu kwa mtu kupeana mkono na mwanamke. Isipokuwa akiwa mke wake au katika wale ambao ni Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1498
  • Imechapishwa: 02/02/2020