Swali: Mimi ni msichana ninayechukia usengenyi na uvumi. Wakati fulani ninakuwa kati ya kundi la watu wanaozungumzia hali za watu na hivyo wanaingia katika usengenyi na uvumi. Mimi ndani ya nafsi yangu nachukia hili. Lakini hata hivyo ni mwenye aibu sana na hivyo siwezi kuwakataza jambo hilo. Kadhalika sipati mahali ili niweze kujitenga mbali nao. Allaah anajua fika kwamba mimi hutamani wabadilishe mazungumzo. Je, ninapata dhambi kukaa pamoja nao?

Jibu: Unapata dhambi katika jmbo hilo isipokuwa ukikemea maovu. Wakikubali nasaha zako ni vizuri. Vinginevyo ni lazima kujitenga nao na kutokaa pamoja nao. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.” (al-An´aam 06:68)

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ

”Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao.” (an-Nisaa´ 04:140)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu basi ayazuie kwa mikono yake. Asipoweza afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu mno.”

Ameipokea Imaam Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Zipo Aayah na Hadiyth nyingi zenye maana kama hii.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/440) https://shrajhi.com.sa/fatawa/40/%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D9%82%D8%A8%D8%A7%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D9%84%D8%A9-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D8%B9%D8%A7%D8%A1-%D9%84%D8%B5%D8%A7%D8%AD%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D8%B1
  • Imechapishwa: 12/01/2020