Mtu anapomuombea maiti anaelekea Qiblah au anamwelekea maiti huyo?

Swali: Je, ni lazima pindi mtu anapomuombea aliyemo ndani ya kaburi kuelekea Qiblah au alielekee kaburi?

Jibu: Haijuzu kuomba du´aa makaburini. Du´aa inaombwa msikitini au nyumbani. Lakini pindi unapomtembelea maiti na ukamuombea du´aa hali ya kuwa hili ni jambo lenye kufuatia matembezi hakuna neno. Katika hali hii unatakiwa kuelekea uso wa maiti na Qiblah umekipa mgongo, umtolee salamu na umuombee du´aa hali ya kuwa hili ni jambo lenye kufuatia. Ama kuelekea Qiblah na kuomba du´aa ni miongoni mwa njia zinazopelekea katika shirki. Du´aa haziombwi makaburini. Hachinjiwi aliyemo ndani ya kaburi.

Anatakiwa kutoa salamu kwanza, aelekee uso wa maiti na aombe du´aa hali ya kuwa hili ni jambo lenye kufuatia salamu. Ama du´aa hali ya kuwa ni kitu chenye kujitegemea ni jambo lisilofaa makaburini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/40/%D8%A7%D8%B3%D8%AA%D9%82%D8%A8%D8%A7%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D9%84%D8%A9-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D8%B9%D8%A7%D8%A1-%D9%84%D8%B5%D8%A7%D8%AD%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%A8%D8%B1
  • Imechapishwa: 12/01/2020