Kuomba idhini kwanza kabla ya kuingia kwa watu

Swali: Ikiwa mwenye nyumba amefungua mlango wa nyumba yake ili awapokee wageni, je, ni lazima niombe idhini au kutoa Salaam kwanza [kabla ya kuingia] au niingie tu moja kwa moja?

Jibu: Hapana. Bora ni kuomba idhini. Kwa kuwa anaweza kuwa na kitu ambacho hataki yeyote akione. Anakuwa na siri na mengineyo. Ujumla wa Hadiyth zinaonesha kuwa ni lazima mtu aombe idhini kwanza katika hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-11-02.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014