Swali: Baadhi ya Suufiyyah huku kwetu wanadai kuwa Maswahabah walikuwa wanajua mambo yaliyofichikana. Je, maneno yao ni sahihi?

Jibu: Wauliza kama ni sahihi ilihali Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ

“Sema: “Hakuna waliomo katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah Pekee. Na wala hawatambui ni lini watafufuliwa”?

Unashaka kwa hili juu ya kwamba sio sahihi? Hakuna anayejua ghaibu isipokuwa Allaah au yule ambaye Allaah amemfunulia kitu katika mambo yaliyofichikana miongoni mwa Mitume Wake:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِ أَحَدًا إِلَّا مَنِ ارْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ

“Mjuzi wa ghaibu na wala hamdhihirishii yeyote ghaibu Yake; isipokuwa yule aliyemridhia katika Mtume.” (07:26-27)

Allaah huwafunulia baadhi ya Mitume Wake sehemu katika mambo yaliyofichikana kwa lengo waweze kusimamisha hoja kwa viumbe. Ama mtu akadai kuwa anajua mambo yaliyofichikana mbali na Mitume, ni kafiri. Kwa kuwa amedai kujua mambo yaliyofichikana. Mwenye kudai kuyajua mambo yaliyofichikana – kama tulivyosoma katika mambo yanayotengua Uislamu wa mtu – anaritadi kutoka katika dini ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020