Kuna fadhilah za kufa al-Madiynah?

Swali: Baadhi ya watu wanasema kufa al-Madiynah kuna fadhila kwa kuwa wewe unakuwa umekufa sehemu ambapo ni karibu na macho ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Hapana. Mtu hatopata isipokuwa matendo yake. Ni mamoja akafa al-Madiynah, akafa mashariki au magharibi. Mtu hana isipokuwa matendo yake. Kuna wanafiki waliofariki al-Madiynah ilihali ndio watu walio kwenye tabaka ya chini kabisa Motoni. Pamoja na hivyo walikufa al-Madiynah na al-Madiynah haitowafaa kitu. Kuna Maswahabah wengi waliokufa mashariki na magharibi ilihali ni Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (03) http://alfawzan.af.org.sa/node/2046
  • Imechapishwa: 18/10/2016